Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Mhe,. George Masaju akiwa katika mazungumzo na Mtaalamu Huru wa Baraza
la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye alibnism Bi
.Ikponwosa Ero wakati alipofika Ofisi kwa Mwanasheria Mkuu na
kubadilishana mawazo kuhusu juhudi na jitihada za serikali katika
kukabiliana na vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenye albinism.
pamoja na changamoto zake.
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Maalum, Julai 19,2017
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Mhe. George Masaju ametoa wito kwa Asasi zisizo za kiserikali ( NGO)
kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ili kupitia ushirikiano huo kukomesha na hatimaye
kumaliza kabisa changamoto zinazowakabili watanzania wenye albinism.
Mwanasheria Mkuu ametoa wito huo
leo ( Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi
Ikponwosa Ero, Mtaalamu Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja
wa Mataifa kuhusu watu wenye albinism
“ Ningependa kutoa shukrani
zako kwa kuamua kuja Tanzania na kukutana na viongozi mbalimbali wa
Serikali, hii ni fursa muhimu kwako ya kupata taarifa sahihi na
rasmi kuhusu jitihada , juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na
serikali na taasisi zake katika kukabili vitendo vya jinai dhidi ya
watanzania wenzetu wenye albinism” akasema Mhe. Mwanasheria Mkuu
Na Kuongeza “ kupitia kwako
nikuombe basi uwahimize viongozi wa asasi zisizo za kiserikali
hususani zile zinazojihusisha na watanzania wenye albinism
kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi yangu na Taasisi
nyingine za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la
kuwasaidia watanzania wenzetu”..
Akasema Serikali inachukulia
kwa uzito wa hali ya juu makosa ya kijinai dhidi ya watu wenye
albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia
wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na sheria kuchukua mkondo wake.
Akasisitiza kwamba Katiba ya
Jamhuri ya Muungano imesisitiza sana juu ya haki ya mtu kuishi na
kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila ya kubagua wakiwamo watu
wenye albinism au ulemavu wa aina yoyote.
“ Haki ya mtu kuishi
imefafanuliwa na kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, na haki hiyo haimbagui mtu mwenye albinisim au mtanzania
yoyote ile na ndio maana makosa ya jinai dhidi ya haki ya mtu kuishi
awaye yeyote yule yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.
Kuhusu takwimu zinazohusu
matukio ya jinadi dhidi ya watanzania wenye albinism,Mwanasheria Mkuu
wa Serikali amesema kwamba tangu mwaka 2006 hadi mwaka huu kumekuwa
na matukizo 66 dhidi ya watu wenye albinisma na huki miaka mingine
ikiwa na haina tukio lolote lile na kwamba kutokana na juhudi
zinazofanywa na serikali matukio hayo yameendelea kupungua kwa kiasi
kikubwa sana mwaka hadi mwaka.
Kuhusu hukumu dhidi ya
watuhumiwa, Mwanasheria mkuu amesema utekelezaji wa hukumu dhidi ya
watuhumiwa wa makoja hayo ya jinai umekuwa wa mafanikio makubwa kwa
zaidi ya asilimi 90 na kwamba hukumu zilizotolewa ni pamoja na
vifungo, huku ya kifo kwa baadhi ya watuhumiwa. Ingawa pia kuna
walioachiwa huru kutoka na kukosekana kwa ushahidi wa kujitosheleza.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ametaja baadhi ya mafanikio mengine ni pamoja na Ofisi yake kuandaa na
kutekeleza uratibu wa uhuishaji wa takwimu za matukio ya kijinai
dhidi ya watu wenye albinism. Uratibu ambao ulifanyika mwaka 2014 kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Wizara ya
Sheria na Katiba na Asasi za Kiraia.
Aidha ametaja mafanikio mengine
ni kuanzishwa kwa dawati maalum katika Divisheni ya Mwendesha
Mashtaka kuhusu watu wenye albinism, kusimamia upepelezi na kuendesha
kesi.
Kwa upande wake Bi. Ikponwosa Ero
akielezea madhmuni ya ziara yake hiyo hapa nchini kuwa , pamoja na
mambo mengine, kutathimini hali ya haki za bindamu za watu wenye
albinisma,, kutathimini hatua na jitihanda zinazofanywa na Serikali
katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye albinism,
kubainisa mapungufu na kuona uwezekano wa kuziba mapengo ya mapungufu
hayo.
Pamoja na kuuliza maswali
mbalimbali kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , maswali na hoja
zilizojibiwa na Mwanasheria Mwenyewe, pamoja na Mkurugenzi wa
Divisheni ya Katiba na Haki za Binadamu na Mkurugenzi Msaidizi kutoka
Divisheni ya Mashtaka, Mtaalamu huyo amemshukuru Mwanasheria Mkuu kwa
kutenga muda wa kukutana naye na kwa maelezo na taarifa zikiwamo za
kitakwimu ambazo zimewasilishwa kwake. Pamoja na kutambua juhudi za
serikali katika eneo hilo.
Bi. Ikponosa Ero aliteuliwa na
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa June 15, 2015 kuwa
Mtaalamu Huru wa haki za bindamu kwa watu wenye albinism.
Imetolewa na Kitengo cha Mwasiliano
Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali
Dar es Salaam
Tags
ALBINISM