Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Ali Hassan Mwinyi
ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka
1985 mpaka 1995 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania
kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti
nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Bi.
Fatma Karume kwa niaba ya Hayati Mhe. Abeid Amani Karume ambaye alikuwa
Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye alikuwa
mstari wa mbele katika kuhimiza shughuli za Vijana wa skauti katika
visiwa vya Unguja na Pemba kwenye sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini
zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais
Mstaafu wa Awamu wa Sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amani
Abeid Karume ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania
kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti
nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa skauti tangia
shuleni na alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika ambapo
mwaka 2001 alipendekeza kuwe na siku ya SKAUTI AFRIKA itakayokuwa
inaadhimishwa kila tarehe 13 mwezi Machi .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa sherehe za miaka
100 ya Skauti Tanzania kwenye ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. (Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Tags
SCOUT TZ