BANDA MEDIA BLOG

WAZAZI NA WAKAZI WA KIZOTA DODOMA WAMEPATWA NA KIZUNGUMKUTI BAADA YA KIJANA WALIYEMZIKA SIKU 4 KUIBUKA AKIWA HAI.



Mwarabu aliyedaiwa kuuawa Morogoro akiwapa mikono wakazi wa kata ya kizota waliokusanyika kwa lengo la kuhakikisha kuwa ni kweli yeye

Seif Ramadhan Mwarabu aliyedaiwa kuuawa Morogoro akiswaliwa nyumbani kwao Kizota Dodoma

Seif Ramadhan Mwarabu aliyedaiwa kuuawa Morogoro akiwa na mama yake mzazi Sara Michael wakati wa Duwa maalumu ya kumuombea maaisha marefu PICHA NA JOHN BANDA








Na John Banda, Dodoma
 kijana mmoja aitwaye Seif Ramadhan Mwarabu umri 29 kuibuka akiwa hai siku nne tangu kufanyika kwa mazishi yake  baada ya uliodaiwa kuwa ni mwili wake kuokotwa maeneo ya Msamvu Mkoani Morogoro na kusafirishwa na ndugu zake mpaka Dodoma kwa mazishi.

BLOG hii ilipiga hodi maeneo ya Kizota hapa Mjini Dodoma kwa lengo la kuzungumza na ndugu zake  ili kupata  ukweli na kuthibitisha kinachosemwa.
Kwanza Mjomba wake Iddi Salum ambaye alitumwa na familia yake kwenda Morogoro kuutambua mwili wa marehemu na kuurudisha nyumbani kwa taratibu za mzishi.

Naye mama yake mzazi Bi Sarah Michael akizungumzia jambo hili ambalo linaleta mashaka na kuacha maswali mengi amesema baada ya mwili kufika kutoka Morogoro aliukagua na kuthibitisha kwamba ni wa mtoto wake lakini alishangaa siku tatu mbele kupokea simu kutoka Dar es salaam  kwa mtoto wake huyo akisema kuwa yumzima wa afya.

Aidha nimezungumza na Seif mwenyewe akisema anashangazwa na taarifa hizo za kifo chake ilihali yeye ni mzima.

Hata hivyo bado wengi wanajiuliza mkasa mzima wa kijana Seif ikionekana kama ni maigizo kwani ni siku kadhaa tu zilizopita walishiriki mazishi yake , lakini sasa wanashangazwa kumuona akiwa mzima kiasi kwamba watu wanamiminika nyumbani kwao kutaka kumuona na kujiridhisha kama kweli ni yeye.

 Hata hivyo kumesomwa Duwa ya kumuombe uhai mrefu kijana Seif iliyoongozwa na shekh wa msikiti wa Kizota Ahmad Suleiman Mkoma ambapo baada ya Duwa hiyo aliwataka ndugu Kumchukulia Marehemu aliyeokotwa mkoani Morogoro na kuzikwa Dodoma kwa jina la Seif Ramadhan Mwarabu kuwa ndugu yao na hivyo kulitunza kaburi lake.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG