BANDA MEDIA BLOG

Baada ya Makonda kutoa agizo, Naye apewa agizo na Rais Magufuli


Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumuagiza aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.


Basi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kufanyia kazi ombi la wananchi la kujengewa kituo cha daladala eneo la Daraja la Nyerere.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Feri jijini Dar es sa laam na kuvuka bahari kwa kutumia cha MV Kigamboni ambapo pia amekutana na wananchi wa Kigamboni.

Hata hivyo Rais Magufuli baada ya kutembelea daraja la Nyerere na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ndio akatoa agizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa huyo kulifanyia kazi ombi la wananchi kuwajenga kituo cha hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG