
Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati ameeleza kuwa tume yake inafuatilia madai yanayotolewa na Odinga kuhusu mfumo unaotumika kutoa matokeo ya Urais, pia wameagiza kuletewa fomu zote namba 34A na 34B kutoka kaunti zote ili kulinganisha matokeo yanayotoka.
Pia Chebukati ameeleza kuwa tume hiyo ina siku 7 za kutangaza matokea na leo ni siku ya 2 , bado wanasiku 5 za kutangaza matokea kwa hiyo kila kitu kitaenda vizuri.
Tags
UCHAGUZI KENYA