Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na
waandishi wa habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10
kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi
Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya
China.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikagua kwa
kujaribu kuziendesha Pikipiki hizo za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa
Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni
ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
.Muonekano wa pikipiki hizo.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea
Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye
thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa
Pikipiki ya TONGBA ya China.
Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo
na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza
Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa
Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa
kutoa Pikipiki hizo.
Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji
kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya
kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za
kawaida 200 Computer 100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya
Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.
Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi
kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika
kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia
Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.
Agizo hilo limekuja baada ya hivi juzi msamariamwema kutoa
taarifa za uwepo wa muhusika wa dawa za kulevya na Askari walipofika
kwenye Hotel wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda mtuhumiwa
akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel na kufanya fujo kumtafuta alietoa
taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV
wakawabainu Askari hao.
Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi
akiwa Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na
kuwalazimisha watoe kiasi cha Million Tano iliwasisambaze picha hizo
kitendo ambacho ni kinyume Sheria ambapo Makonda awezi kuruhusu vitendo
hivyo votendeke kwenye Mkoa wake na kueleza kuwa anataka Sheria na Haki
vitendeke.
Makonda kubaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege
wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na
Askari wanawabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu
kwenye sehemu za mapumziko.
Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda
kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya
Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.
Tags
MAKONDA