Makamu wa Rais wa Startimes
Tanzania,Ms Zuhura Hanif akizungumza na waandishi wa habari pamoja na
wadau wa soka wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa
msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Startimes
Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na
wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano
wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu Maarufu kwa jina la Sharobora wa
Kichina akielezea namna kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya
Bundesliga
Mhariri mkuu wa gazeti la
Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu ligi ya Bundesliga
itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwenye uzinduzi huo uliofanyika
leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali nchini.
Picha ya pamoja ya waandishi wa habari na Meza Kuu ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Ms Zuhura Hanif
PICHA NA ROBERT OKANDA
……………………………..
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog
Kampuni ya Startimes nchini
Tanzania imezindua msimu mpya wa kuonesha Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu
kwa jina la ‘Bundeslinga wa mwaka 2017-18 ambapo mechi zote 300
zitarushwa live kupitia ving’amzi vya Startimes kupitia chanel tofauti
zinazoonesha Mpira wa Miguu.
Uzinduzi huo umefanyika leo jijini
Dar es salaama na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wanaofatilia Mchezo
wa Mpira na pia lengo kubwa ni kuwafahamisha wapenzi wa soka nchini
kuanza kununua ving’amuzi na kujiunga na vifurushi hivyo kwa ajili ya
kuona mechi hizo ambapo pazia la ligi hiyo litafunguliwa siku ya Ijumaa
Mabingwa watetezi Bayern Munich watawakaribisha Bayern Leverkusen.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania,Ms Zuhura Hanif amesema kuwa
kuna fursa kwa waandishi wa habari za michezo kufanya mashindano ya
uandishi wa mechi hizo za Ligi Kuu ya Ujerumani na mwandishi
atakaeibuka mshindi wa shindano hilo atapata fursa ya kwenda nchini
Ujerumani kushuhudia mechi na atakagharamikiwa kila kitu na Startimes.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa
Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu kwa jina la utani
Sharobaro wa Kichina amesema kuwa wana mahusiano mazuri na bundesliga
kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu
kuonyesha ligi hiyo.
Aidha Meneja Uwendeshaji
Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa huduma mpya ya malipo kwa wale
wenye hali ya chini wanaweza kulipia siku moja king’amuzi cha
Startimes kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia
elfu 4000.
Tags
BUNDESLIGA 2017-18