Afisa mahusiano wa TECNO Mobile
Eric Mkomoya (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na kampeni ya WashaCheche ns kumkabidhi Raymond Msenga (Jay
Mond) wa pili kutoka kushoto zawadi ya simu toleo lao jipya kabisa la
simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni iliyopewa kuifanya wiki
mbili zilizopita.

Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni akikabidhiwa simu na meneja wa masoko mtandaoni Chen Bo simu mpya aina ya TECNO SPARK.

Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya akiwaonyesha waandishi wa habari toleo jipya la simu zao kabla ya kumkabidhi Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni.
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog
KAMPUNI ya simu za TECNO imemzawadia zawadi ya simu mchekeshaji Raymond Msenga maarufu kama JayMondy ikiwa ni toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni aliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Mahusiano wa
kampuni hiyo Eric Mkomoya alisema “nia na madhumuni ya kampuni yetu ni
kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania kupitia simu hii mpya, vijana
wanaotaka kufanikiwa wanapitia vikwazo vingi, ila Tecno inataka
kuwasaidia kupitia washa cheche.” KAMPUNI ya simu za TECNO imemzawadia zawadi ya simu mchekeshaji Raymond Msenga maarufu kama JayMondy ikiwa ni toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni aliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.
Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni aliomba simu kutoka Tecno Mobile kupitia video zake ili aweze kurekodi kwa ubora mzuri. Tecno Mobile walisikia kilio chake na kumpa zawadi ya simu mwaka mzima kwa kila toleo.
“Nimefurahi kupata zawadi ya simu hii, na kikubwa na ni nafasi ya kupata mfululizo wa matoleo yote mapya ya simu zao, nawasihii vijana wenzangu wenye vipaji wawashe cheche zao na wanaweza kupata msaada kutoka Tecno Mobile.” Alisema Raymond Msenga maarufu kama Jaymond.
Meneja wa masoko mitandaoni wa TECNO, Kelvin Boniface alisema “Namna ya kushiriki katika kampeni hii ni rahisi, Upload video au picha Kwenye mitandao ya kijamii ukitumia hashtag #WashaCheche bila kusahau kutuTag “Tecno Mobile Tanzania kwenye mitandao yetu ya kijamii ya twitter, Facebook na Instagram” alisema
Kampeni hii itasukumwa na simu yao mpya aina ya TECNO SPARK (TECNO CHECHE) ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiletea maendeleo na kujikwamua kimaisha.
Tags
TECNO SPARK