Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imekusudia kuboresha huduma zake pamoja kuzisogeza
karibu zaidi na wananchi ambao ndio wateja wakubwa wa Sekta hiyo. Hii ni
katika kuboresha utoaji huduma na kuongeza ufanisi wa huduma za Ardhi.
Katika kuhakikisha hili
linafanikiwa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaanzisha
mifumo ambayo itakuwa inatumika kama njia rahisi ya utoaji huduma kwa
wananchi. Mifumo yote hiyo ni kwa lengo la kuboresha huduma, kurahisisha
huduma na pia kuondoa urasimu ambao ungeweza kujitokeza katika utoaji
wa huduma kwa mwananchi.
Mfumo wa GePG (Government electronic Payment Gateway)
ni mfumo wa Serikali ambao umetengenezwa kwa lengo la kukusanya na
kusimamia mapato ya Serikali. Mfumo huu pia utakuwa unatumiwa na Wizara
kuu za Serikali, Taasisi za kifedha, Makampuni ya simu, Serikali za
mitaa na Idara zote za Serikali ambazo zina vyanzo vya mapato.
Malipo yote yatakuwa yanalipwa kwa kutumia namba maalumu ya malipo inayojulikana kama “control number” ambayo itamuwezesha mwananchi kulipia katika benki za NMB, CRDB au kwenye Mpesa na Tigo pesa mahali popote.
Mwananchi anaweza kupata
makadirio yake ya kodi ya pango la Ardhi kwa kutumia mfumo huu wa GePG.
Hii ndiyo maana halisi ya kusema sasa huduma za sekta ya Ardhi
zinaboreshwa kwa kuondoa usumbufu wa kutembelea vituo vya makusanyo.
Njia mojawapo ya kupata makadirio ni kwa kutumia tovuti ya Wizara ya Ardhi (www.ardhi.go.tz).
Utachagua ‘kadiria kodi ya Ardhi’ na kisha utafuata maelekezo ya namna
ya kuingiza taarifa za kiwanja chako. Baada ya kuingiza taarifa sahihi
utabonyeza kitufe cha kadiria na hapo utapata taarifa za deni la kodi ya
pango la ardhi pamoja na namba ya kulipia inayoanzia 99117…..
Pia unaweza kupata makadirio ya
kodi ya pango la ardhi kupitia simu ya mkononi kwa kuingiza menyu kuu
ya taifa ambayo ni *152*00# , kisha unachagua namba 4 malipo ya
Serikali. Baada ya hapo utachagua namba 2 kadiria kodi ya kiwanja
ambapo, utachagua nmba 1 kwa viwanja vya Dar es Salaam au namba 2 kwa
viwanja vya mikoa mingine. Utachagua 1 kama unajua namba ya kiwanja au 2
kama unajua Lot ID na hapo hapo utapokea ujumbe wa malipo ukiwa na
kumbukumbu namba inayoanzia na namba 991177….. Ukishapokea huo ujumbe
utakuwa na uwezo wa kulipia katika beki za CRDB, NMB na kwa Mpesa au
Tigo pesa.
Malipo yoyote yakifanyika kupitia
simu ya mkoni, mwananchi atapokea uthibitishpo wa malipo ambao ni
risiti namba. Nakala ngumu ya risiti (hard copy) inapatikana
katika kituo chochote cha makusanyo, mwananchi atapaswa kwenda na
uthibitisho wake wa malipo tuu ili kupatiwa nakala ngumu ya stakabadhi.
Tags
William Lukuvi