Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta na Makamu wa
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Michael Wambura
(kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa TFF uliofanyika
leo katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma
: Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia (kulia) akiapa mbele ya Wakili na
Msajili wa Vyama vya Michezo nchini Bw. Ibrahimu Mkwawa (aliyesimama
kushoto) baada ya kutangaza mshindi wa nafasi hiyo leo katika Ukumbi wa
St. Gasper Mkoani Dodoma
Mwakilishi wa TFF kutoka zoni
namba nne Bi. Sarah Chao (kulia) akiweka sahihi katika kiapo alichoapa
baada ya kutangaza mshindi leo wakati wa Mkutano Mkuu wa TFF Mkoani
Dodoma. Kushoto aliyesimama ni Wakili na Msajili wa Vyama vya Michezo
nchini Bw. Ibrahimu Mkwawa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu
Wizara ya hiyo Pro. Elisante Ole Gabriel (katikati) wakifuatilia uapisho
wa viongozi wapya wa TFF waliochagulia leo katika Mkutano Mkuu wa TFF
Mkoani Dodoma
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa TFF
(hawapo pichani) baada ya kutangazwa na kuapishwa kwa viongozi wapya wa
TFF leo Mkoani Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia akitoa neno la shukrani kwa
wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF kumwezesha kushika nafasi ya urais leo
wakati wa Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika katika Ukumbi wa St. Gasper
Mkoani Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM
………………………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Uongozi mpya wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umetakiwa kufikia Januari mwakani
kuwajibika kama mashirika mengine ya mpira wa miguu duniani
yanavyowajibika kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti
ili wananchi wapate fursa ya kufahamu namna fedha zinavyopatikana na
jinsi zinavyotumika katika kuboresha na kuendeleza usimamizi bora wa
soka nchini.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati
wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
na leo katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma
Aidha Mhe. Mwakyembe amewapongeza
viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne kwa
kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa pamoja katika kutekeleza
majukumu yao ya kila siku huku akiwapongeza washiriki wote waliothubutu
kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF
wa mwaka huu.
Kwa upande wake Rais mpya wa TFF
Bw. Wallace Karia amewaahidi wapiga kuwa wake kufanya kazi kwa weledi wa
hali ya juu kwani nafasi aliyopewa na wajumbe hao kwa kumuamini ni deni
ambalo atalilipa kwa kuleta mafanikio makubwa katika mchezo wa soka.
Bw. Karia amesema kuwa furaha
waliyonayo viongozi wote waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka
minne iende kuwa furaha ya kazi kwa kufanya yale watanzania wanatarajia
kutoka kwao.
Tags
Uchaguzi TFF