Simba imeishinda Rayon Sports kwa bao 1-0 katika mechi nzuri ya kirafiki iliyokuwa maalum kwa ajili ya tamasha la Simba Day.
Tamasha
hilo ambalo hufanyika kila Agosti 8 ya kila mwaka lilifana kwa mambo
mbalimbali ikiwemo kutambulishwa kwa wachezaji wapya wa Simba.
Simba walianza kupata
bao dakika ya 24 likifungwa na kiungo hatari kwa sasa Ibrahimu Mohamed
‘MO’ aliyepokea pasi safi kutoka kwa Emmanuel Okwi na kuwa chambua
mabeki wa Rayon ambayo iliweza kuwaacha wachezaji sita muhimu ambao wapo
kwenye timu ya Taifa ya Rwanda inayojiandaa naa Chan dhidi ya Uganda.
Hadi mapumziko Simba
walikuwa mbele kwa bao hilo moja na kipindi cha pili timu zote zilifanya
mabadiliko Simba ikimuingiza kiungo wao hatari Haruna Niyonzima kipenzi
cha wana Yanga aliyehamia Msimbazi na alionesha uhodari mwingi kwa
kuuchezea Mpira kwa madaha.
Kama Simbaa wangekuwa
makini wangeweza kutoka na ushindi mnono kwani mshambuliaji wao hatari
John Bocco aliweza kukosa nafasi mbili za wazi akiwa yeye na golikipa
hadi mpira uanaisha Simba wameibuka na ushindi wa bao 1-0 na kusherekea
vizuri siku yao ya Simba Day ambayo imetimiza miaka tisa tangu
kuanzzishwa.
Tags
SIMBA SC