Timu ya Simba SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na
wenyeji, Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan,
Zanzibar usiku wa leo.
Mlandege ambayo ilifungwa 2-0 na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC Jumapili usiku, leo ilikuwa mwiba kwa washindi wa taji la Azam Sports Federation Cup.
Mlandege ambayo ilifungwa 2-0 na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC Jumapili usiku, leo ilikuwa mwiba kwa washindi wa taji la Azam Sports Federation Cup.
Simba ikicheza bila ya
nyota wake wawili Emmanuel Okwi na John Bocco imeshindwa kuonesha
cheche za kutikisa mabao huku ikiendelea kusuwasua katika suala
umaliziaji.
Simba ambayo imecheza
mechi mbili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kutoka na
ushindi wa goli 1-0 ikizifunga timu za Rayon Sport ya Rwanda na Mabingwa
wa Zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom 1999-2ooo Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Pamoja na mabadiliko
yaliyofanywa na Omog kipindi cha pili, lakini hakuwatumia kabisa Okwi na
Bocco kuashiria amewapumzisha kwa ajili ya mchezo ujao Jumatano dhidi
ya mahasimu wa jadi, Yanga kuwania Ngao ya Jamii.Simba SC imeweka kambi kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Na watani wao wa jadi, Yanga nao wapo kisiwani Pemba kwa malengo hayo hayo.
Kikosi cha Mlandege kilikuwa; Masoud Kombo, Adam Hamad, Amir William, Abubakar Mwadini, Abubakar Omar, Hassan Ramadhani, Edwin Charles, Nicholaus Frank, Shaaban Amir, Jaffar Rajab na Mohammed Abdallah.
Simba SC; Aishi Manula, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali, Jonas Mkude/James Kotei dk76, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk84, Mohammed Ibrahim, Laudit Mavugo/Juma Luizio dk62, Haruna Niyonzima na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Jamal Mnyate dk68.
Tags
SIMBA SC