Wakinamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya ya Dhahabu
Baadhi ya vijana wa kijiji cha Sambaru
…………………………………………………………….
Na Woinde Shizza,Singida
Zaidi
ya vijana 60 wa kijiji cha Sambaru kata ya Ikungi wilayani Ikungi
mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya Sambaru Gold
Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo ya kazi waliyokuwa
wakimfanyia mgodini kwake
Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa
kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo hajawalipa hela zao na badala yake amewafukuza kazini hapo bila
kuwalipa malipo yoyote .
kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo hajawalipa hela zao na badala yake amewafukuza kazini hapo bila
kuwalipa malipo yoyote .
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi
wa kijiji lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika kuwasaidia kwa majukumu mbalimbali ya kifamilia.

“Tumekuwa
tunamfata muwekezaji huyu na kumuomba atulipe fedha zetu lakini
amekuwa anatukana na kusema hatudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia
hatua ya kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka
polisi,”alisema Saidi
Kwa upande wake kijana mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi
kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikubali na akaahidi kuwalipa na aliomba muda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo umepita na hadi leo vijana hao hawajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisa.

Alipotafutwa mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan ili kubainisha kama ana taarifa za vijana hao
nae alisema kuwa ni kweli ana taarifa za vijana hao na alishamtumia mmiliki wa kampuni hiyo taarifa za madai ya vijana hawa lakini hajateleza hivyo ameamua kupeleka swala hili katika ngazi za juu ili wamsaidie

“Sisi
kama kijiji tumekuwa tuna utaratibu wa kuwapa vijana wawekezaji hawa
na hii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta mwekezaji anataka
vijana wa kumsaidia kazi huko mgodini kwake analeta barua katika ofisi
ya kijiji na sisi tunampa vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa
mwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya
kazi mgodini kwake lakini hajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifuatwa
anasema kuwa hadaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa
kijiji nikishirikiana na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana
hawa walipwe hela zao na hadi sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa
wilaya”alisem Mwenyekiti wa kijiji Mfaume Hassan
“Mimi
sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana wangu wote ambao nawaajiri
nawalipa vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda
kijijini kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema hivi kama
kuna mtu ambaye ananidai afuate sheria ,aje na vielelezo anidai na
kama ni kweli nitamlipa ila sidaiwi na mtu yeyote “alisema Magoma
Akiongelea swala hilo Mkuu wa wilaya
ya Ikungi Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo
alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao
pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia
barua ya kumuita ofisini kwake mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .

Tags
MWEKEZAJI