VITU 6 USIVYO VIJUA KUHUSU KISIWA CHA GUAM NA AMBAVYO VITAKUSHANGAZA
byJohn Banda-
0
Sio kila mara unasikia kuhusu kisiwa cha Guam ambacho ndio kikubwa zaidi katika bahari ya Pacific na kinamilikiwa na Marekani.
Kimekuwa
katika habari kwa sababu Korea Kaskazini imetishia kushambulia kambi
yake ya kijeshi ikiwa ni miongoni mwa mgogoro na Marekani.
Inajiri baada ya rais Donald Trump kusema kuwa taifa hilo linafaa kutarajia vita vikali kutoka kwa Marekani.
Huku Guam ikiangaziwa haya hapa mambo sita unayofaa kujua kuhusu kisiwa hicho.
Ni eneo ambalo liko mbali zaidi kwa raia wa Marekani kutembelea bila kutoka Marekani.
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption Eneo la Tumon Bay ni maarufu miongoni mwa watalii Licha
kumilikiwa na Marekani, kiko maili 8000 kutoka Marekani na inachukua
takriban saa 19 kusafiri kwa ndege kutoka mji wa New York.
Wamarekani wanaweza kuelekea katika kisiwa hicho bila kutumia pasipoti.
Kila mtu aliyezaliwa kisiwani Guam ni Mmarekani lakini hawezi kumpigia kura rais.
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption Sherehe inafanyika katika baranara mjini Tumon Tangu
mwisho wa vita vya dunia , watu wawili waliokuwa wakiishi katika kisiwa
hicho walipewa uraia lakini hawawezi kumpigia kura rais wa Marekani.
Wana mwakilishi mmoja wa serikali laki yeye hana uwezo wowote kuhusu
utengenezaji wa sera. Guam ni kambi muhimu ya kijeshi
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption Ndege ya kijeshi ya Marekani inapaa kutoka Guam Robo ya kisiwa hicho kinamilikiwa na jeshi la Marekani na kinatumiwa kama kambi ya wanamaji na wanaanga
Pia inakadiriwa kwamba karibia asilimia 10 ya watu wa Guam wenye idadi ya 160,000 ni ya wanajeshi.
Raia wa Guam wanajulikana kama Chamorro.
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption Guam ni kisiwa cha kisasa chenye majumba marefu na maeneo manne ya kitalii Chamorro
ni jina la jumla linalopewa watu wanaoshi katika kisiwa cha Guam na
watu wanaoshi katika visiwa vya Micronesia katika bahari ya Pacific.
Utamaduni
wao unafanana na ule wa Uhispania zaidi ya Umarekani kwa sababu
Uhispania ilidhibiti kisiwa hicho kwa takriban miaka 300 hadi 1898.
Watu katika eneo hilo hawatozwi kodi
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption Tumon ndio wilaya ya kutalii kisiwani Guam Watalii
kutoka Taiwan , Korea Kusini na Japan huchukua saa nne kusafiri hadi
katika kisiwa hicho kwa likizo ya kupata jua mbali na kununua vitu
ambavyo havilipishwi kodi.
Maduka yote makubwa huuza bidhaa za mitindo na mengi hufunguliwa kwa saa 24 kwa siku. Ricardo Blas Jr. ndio mtu maarufu zaidi katika kisiwa cha Guam
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption Blas Jr. akishindana katiika michezo ya olimpiki ya 2012. Mtu
huyo mwenye umri wa miaka 30 ni mchezaji wa judo ambaye alishiriki judo
katika michezo ya Olimpiki ya 2008 na 2012 na alibeba bendera ya Guam
katika mashindano yote lakini akashindwa kupata medali licha ya kuwa
mhcezaji judo mwenye uzani mzito zaidi wa kilo 214.
#BBCswahili