Waziri wa michezo nchini
Tanzania Mh.Dk Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto
waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya
kucheza mpira wa miguu katika academy ya klabu ya Manchester City
nchiniUingereza.
Malimi Majaliwa wa kwanza
kushoto na Daudi DAmasi wakiwa katika picha ya pamoja baada yakupewa
Baraka za safari na Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo
Dk. Harrison Mwakyembe)
Akiongea katika hafla hiyo fupi
kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya
Tecno Mobile Bwana, Eric Mkomoya alisema kua kampuni ya Tecno Mobile
ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon
Cxto leo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda
kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia endapo watafanya
vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo. ,(wadhamini wa kuuwa safari
(Wazazi na walezi wa vijana
wanaokwenda Manchester city wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini
wa kuu kutokea Tecno Mobile.)
Alisemaa . ”Tumefurahi kukutana na
serikali hasa Waziri wa michezo na kuamua kuwapa Baraka zake vijana
wetu wanaokwenda huko wataondoka usiku wa tarhe 23 na kurudi tarehe 30
mwezi wa nane”.
Akikaribishwa na mkurugenzi wa
michezo, waziri wa michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kua serikali
ina furaha kuona wadau wanajitokeza kukuza vipaji nchini Tanzania, hasa
kwa watoto wanao chipukia.
Dk Harrison Mwekyembe pia amesema
“niwaombewa dau katika sekta ya michezo tushirikiane katika kukuza
michezo, na washukuru kampuni ya Tecno Mobile kwa kuonesha juhudi za
wazi katika kufanikisha hili, serikali pia inafanya jitihada kwa nafasi
kuhakikisha viwango vya soka na michezo kwa ujumla vinakua.”alimaliza.)
Mzazi wa mtoto mmoja wapo Malimi,
Majliwa Mbasa amesema anafuraha kuona kijana wake amepata nafasi hiyo
anaamini atafanya vizuri liafungue milango kwa vijana wengine wadogo wa
kitanzania walioko nchini waweze kwenda kucheza soka la kulipwa nchini
uingereza.
Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja
na Malimi Majaliwa wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata
nafasi hizo kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile naasasi ya michezo
ya Magnet, watoto hao ambao wote wana miaka kumi na mbili wataondoka
kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini
tarehe 30.
Msafara huo utaongozwa na wazazi
na walezi wa watoto hao akiwemo kocha mwenye utalaamu wa kulea vipaji
vya vijana kocha Juma Maswanya. Tecno mobile ndio wadhamini wakuu wa
safari hii wanajumuisha vijana kutoka nchi za afrika ambako kampuni hii
inapofanyakazi hivyo Nigeria, misri ,Tanzania, Ghana pamojana Kenya
Afisa Mahusiano wa Tecno Mobile Eric Mkomoya wa kwanza kushoto, meneja Masoko Franck Luo, wa kwanza kulia)
aziriwaHabari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na
watoto wawili Daudi Damasi na Malimi Majaliwa wanaokwenda kufanya
Majaribio,
Tags
MAN CITY