BANDA MEDIA BLOG

DEREVA WA LISSU BADO ANASAKWA NA JESHI LA POLISI, 17 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI


Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani sale za Jeshi la Wananchi zilizokuwa zikitumika kinyume na utaratibu

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Murotoakifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari kuhusu watu 17 ambao wamekamatwa na jeshi hilo huku wakiwa na vifaa mbalimbali zikiwemo nyara za serikali [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]



Gari alolikua akitumia Tundu Lisu likiwa pamoja na magari mengine nje ya ofisi za Polisi Mkoa wa Dodoma

Na JOHN BANDA
-DODOMA

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema bado linaendelea kumtafuta dereva wa Tundu Lissu,Simon Bakari Mohammed huku likimtaka popote alipo ajisalimishe katika Kituo chochote cha Polisi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Mjini hapa,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Gilles Muroto alisema wanaendelea kumtafuta dereva huyo kutokana na kuwepo wakati tukio la kupigwa kwa risasi kwa Lissu linatokea.
 “Bado hatujampata lakini tunaendelea kumtafuta popote alipo tunamwambia tunamtafuta ila bado hatujampata tunaendelea kwa kuvitumia  vyanzo vyetu,”alisema
Alipoulizwa kuhusina na magari nane aina ya Nissan wanayoyashikiliwa na Jeshi hilo,Kamanda Muroto alisema bado wanaendelea kuyashikilia mpaka watakawapata wahusika wa tukio hilo.
 “Magari tunaendelea kuyashikilia kikubwa tunataka usaidizi ili tuweze kuweka mambo yetu sawa,”alisema

Kuhusina na ulinzi nyumbani kwa Lissu,Kamanda Muroto alisema,Usalama upo wa kutosha kutokana na Jeshi hilo  kuuimarisha .
“Pia tumeweka Road Bloak, Mji uko ndani ya bakulia umezibwa na doria za magari na pikipiki sehemu zote za kutoka na kuingia Dodoma zipo katika doria,”alisema
Alipoulizwa ni kampuni gani inalinda katika eneo Lissu alipopigiwa risasi,alisema hawezi kujua ila anachojua ni kwamba kila nyumba ina mlinzi binafsi.
“Kila nyumba ina ulinzi binafsi  lakini ulinzi wa getini upo kama kawaida sema siwezi kujua ni kampuni gani inafanya ulinzi huo,”
BANDA BLOG ilifika kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na kukuta gari la Lissu likiwa nje ya Jengo hilo huku likiwa limefunikwa upande   ambao una matundu ya risasi ambapo pia namba za gari hiyo zikiwa zimetolewa.
Wakati huo huo Jeshi linawashikilia watu watano raia wa China kwa  kupatikana na nyara za Serikali ambazo ni Magamba ya 652 ya Kakakuona,Kucha na jino la Simba  kinyume cha sheria.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 11 mwaka huu kwa kushirikiana na askari wa kikosi dhidi ya Ujangili(KDU) Kanda ya Kati Manyoni.
Kamanda Muroto alisema  watuhumiwa hao walikamatwa na Magamba 652 ya mnyama Kakakuona,kucha tano za Kakakuona,kucha nne za Simba, na jino moja la Simba.
“Katika msako unaoendelea maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wamekamatwa watuhumiwa 12 kwa makosa ya uvunjaji wa nyumba na wizi,maliz ilizokamatwa ni Television Flat Screen 13 Radio Saboofer 2,Speaker 5,Deck ,bhangi kete 12,”alisema
Kamanda Muroto,alitoa wito kwa wote walioibiwa majumbani mwao kufika katika Kituo cha Polisi cha kati kwa ajili ya kutambua mali walizoibiwa.
mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG