
Azam na Simba ndio timu pekee ambazo hazijaruhusu nyavu zao kutikiswa kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara msimu mpaka sasa.
Morris alisema wamejiwekea malengo msimu huu ya kuhakikisha wanaweka rekodi ya kuwa timu ambayo haijaruhusu bao msimu huu ingawa amekiri si kazi nyepesi lakini bidii na kujituma inawasaidia kutimiza malengo yao.
" Hakuna kingine kiinachoibeba safu yetu ya ulinzi kama umoja tulionao na kila mmoja kujua nini anatakiwa kufanya na kusaidiana.Hali hii imetufanya kutengeneza ukuta wa chuma ni ngumu kupitika kirahisi.
Tags
Azam fc