| Mkuu wa Maimamu wa Msikiti wa Nunge Shekh Ahmed Zuber akifafanua jambo wakati akitoa mawaidha katika uwanja wa jamhuri wakati wa sherehizo |
| Mawadha yakiendelea |
| Waumini wa Dini ya Kiiislamu Wakisujudu wakati wa swala hiyo ikiendelea [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA, BLOG |
| Shekh Zuber na Mjukuu wake Baada ya Ibada ya Eid el hajj 2017 |
JOHN BANDA-DODOMA
MKOANI
Dodoma Waislamu wametakiwa kujikita katika malezi ya watoto kwa kuhakikisha
wanawapatia elimu ya dini ya kiislamu kwani itawasaidia katika maadili pamoja
na kuipenda nchi yao.
Hayo
yalilezwa Mjini hapa na Ustadh Abdullaziz Yunus wakati wa Ibada ya swala
ya Idd el hajj iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani hapa.
Ustadh Yunus
ambaye ni Imamu katika Msikiti wa Bilal uliopo Area C Mkoani hapa amesema,
wazazi na walezi wanawajibu wa kuhakikisha watoto wanapatiwa Elimu ya dini ya
Kiislamu kwani itawasaidia katika maadili pamoja na kuipenda nchi yao.
Amesema kitendo
cha wazazi kuwaacha watoto wakiendelea kufanya mambo ambayo ni tofauti na dini
kwa kisingizio cha Sayansi na Teknolojia ndio husababisha,watoto hao kuporomoka kimaadili.
Awali Imamu
Mkuu wa Msikiti wa Nunge Shekhe,Ahmed
Zuber aliishukuru Serikali kwa kukubali eneo la Kizota liendelee kutumiwa na
Waislamu kwa ajili ya maziko.
Wakati huo
huo Shekhe wa Jumuiya ya Ahmadiyya
Muslim Jamaaat Tanzania Bashart Ur Rehman Butt amewataka waumini wa dini
ya Kiislamu nchini kuisaidia jamii yenye
mahitaji maalumu kuwa ni sehemu ya tendo la ibada la kila siku badala ya
kusubiri sherehe za Eid el hajj .
Kiongozi huyo wa dini amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ibada ya swala ya
sikukuu ya Eid el hajj
Mbali na hilo amewataka waumini wa dini
hiyo kuendelea kudumisha amani upendo na ushirikiano ili maendeleo
yanayosisitizwa kwa ajili ya Taifa yaweze kuongezeka na hatimaye tufikia hatua
ya kiuchumi wa viwanda na biashara.
mwisho
Tags
EID EL HAJJ 2017