Naibu Waziri Ofisi ya Rasi, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa wataalam wa maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rasi, Tamisemi Selemani Jafo akisikiliza taarifa ya mradi wa maji Mkoyo.
Baadhi ya wajumbe wa kijiji cha
Mkoyo pamoja na wataalam wa maji wa manispaa ya Dodoma wakati wa ziara
ya kikazi ya Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo.
jenerata ya mradi wa maji Mkoyo.
……………………..
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo amesikitishwa na baadhi ya wakandarasi washauri
wanaosimamia miradi ya maji katika halmashauri mbalimbali hapa nchini
kwa kutofanya kazi yao kwa umakini na hivyo kuruhusu wakandarasi wa
ujenzi wa miradi ya maji kujenga miradi hiyo chini ya kiwango.
Jafo alitoa kauli hiyo
alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mkoyo ndani ya Manispaa ya
Dodoma, ambapo amebaini mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Co LTD
hakuwa makini wakati wa utekelezaji wa mradi huo kwani imeonekana mradi
huo ukiwa na changamoto kadhaa licha fedha nyingi kutumika zaidi ya
milioni 430 kati ya milioni 480 zilizipangwa kwa mradi huo.
Amesema wakandarasi hao wamekuwa
wakisababisha miradi kujengwa chini ya kiwango na kusababisha kushindwa
kuwapatia maji wananchi kama ilivyotarajiwa.
Aidha amebaini kampuni hiyo mshauri huyo ndiye yule yule aliyesimamia mradi kijiji cha Itiso ambao
aliutembelea mradi huo mwezi Agosti mwaka huu na kukumbana na changamoto nyingi.
Kufuatia hali hiyo, Jafo
amemuagiza Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhandisi Enock
kwa shirikiana na wahandisi wa maji wa halmashauri za mkoa wa Dodoma
kufanya tathmini ya miradi yote ya maji inayosimamiwa na mshauri huyo
ili Ofisi ya Tamisemi ifanye maamuzi sahihi.
Aidha amesema serikali haitaweza
kuvumilia endapo ikibainika mshauri wa miradi hiyo ameshindwa kuisaidia
serikali katika miradi ya maji anayoisimamia.
Naibu waziri Jafo amezitaka
kampuni zote za washauri waelekezi kutimiza wajibu wao katika kusimamia
miradi ya maji kwani wananchi wamekuwa wakitaabika sana kutokana na kero
ya maji ilihali wao wamechukua dhamana ya kusimamia miradi hiyo ya
serikali.
Tags
WAKANDARASI