Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa majengo ya shule Manispaa ya Dodoma
Moja ya nyumba ya walimu iliyojengwa katika shule ya msingi Nzasa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ihumwa
alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na vyoo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Ihumwa.
…………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote kukamilisha
miradi ya ujenzi wa madarasa, mabweni, vyoo, maabara, na miundombinu
mingine ya shule za msingi na sekondari kabla tarehe 30 Novemba mwaka
huu.
Jafo aliyasema hayo leo hii
alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi hiyo katika shule ya Nzasa na
Ihumwa zilizopo katika manispaa ya Dodoma.
Mnamo mwezi Juni serikali ilitoa
fedha kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (P4R) sh.bilioni 16 kwa ajili
ya miundo mbalimbali kwa shule 63 za sekondari na shule 56 za msingi
katika halmashauri mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kufundishia na
kujifunzia.
Hata hivyo bado kuna halmashauri
chache zinasuasua kukamilisha ujenzi huo hali iliyomlazimu Naibu Waziri
huyo kuagiza halmashauri zote hapa nchini kukamilisha miradi iliyo
pangwa katika maeneo yao kabla tarehe hiyo.
Jafo amesema kwamba hataki kusikia
au kuona halmashauri yeyote ambayo itakuwa haijakamilisha miradi hiyo
kwa kipindi kilichopangwa.
“Hatua kali itachukuliwa kwa yeyote atakayefanya uzembe ambao utasababisha ujenzi huo kutokamilika,”amesema Jafo
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri
Jafo amelipongeza sana jeshi la wananchi kutoka kikosi cha Ihumwa kwa
kushirikiana na manispaa ya Dodoma kwa kufanikisha ujenzi katika shule
ya Nzasa na Ihumwa na ameviomba vikosi vingine hapa nchini kuiga mfano
huo mzuri ambao umewezesha kukamilisha miundombinu hiyo kwa gharama
ndogo.
Jafo anaendelea na ziara zake za kikazi za kukagua miradi ya maendeleo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Tags
ELIMU