BANDA MEDIA BLOG

Jini Mkata Kamba Azidi Kumvaa Manji Leo Avuliwa Udiwani Rasmi


Jini Mkata Kamba Azidi Kumvaa Manji Avuliwa Udiwani Rasmi
Mfanyabiashara Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema hayo leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari.

Kutokana na hilo wamemuondoa Manji kwenye nafasi hiyo kutokana na kukosa sifa.

Chaurembo amesema amemwandikia Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kuhusu suala hilo ili aweze kupanga uchaguzi mwingine.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG