Mshambuliaji
mpya wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette jana jumatatu usiku
alifanikiwa kuifungia mabao 2 – 0 dhidi ya West Bromwich Albion katika
mchezo wa Ligi kuu ya England , kwa bao la dakika ya 20 kipindi cha
kwanza na bao lingine la dakika ya 67 kipindi cha alilofunga kwa njia ya
penati.
Alexandre Lacazzete mpaka sasa
amevunja rekodi ya Brian Marwood iliyowekwa mwaka 1988 ya kufunga katika
michezo mitatu ya mwanzo ya ligi ya Epl. Kwa matokeo hayo yanawafanya
Arsenal kubaki katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu Uingereza
wakiwa na alama zao 10 huku Manchester City wakiwa kileleni.
Lacazzete amefikisha jumla ya
magoli manne tangu msimu wa Ligi Kuu ya England uanze aliposajiliwa
akitoka Lyon ya nchini Ufaransa kwa kitita cha rekodi ya klabu
Tags
ARSENAL