Kwanza naanza kwa kusema nampa pole ndugu yangu, mTanzania mwenzangu
Tundu lissu kwa majanga yaliyo mpata, mimi ni mkristo miongoni mwa mambo
ambayo Yesu alisema na ni kauli yake ya mwisho ni Duniani mnayo dhiki
alikuwa anamaanisha matukio kama haya kwamba kuna watu watanyimwa haki
ya kuishi kwa sababu ya misimamo yao,
na utu wao utapuuzwa kwa sababu ya
misimamo yao, wataonewa kwa sababu ya mitazamo yao, hii ni Dunia
matukio kama haya hayajaanza leo na wakati wote watekelezaji wa matukio
kama haya wanaishia pabaya wakati utawahukumu. Ninacho muombea ndugu
yangu apone haraka na Mungu amsaidie. Mungu ibariki Tanzania, Mungu
ibariki Afrika