Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri
ya Ilala ambaye pia Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto
ameeleza sababu zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa
cheo cha nyota nne na serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa
miongoni mwa Zahanati tano zilizofuzu.
Akizungumza mara baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi
Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza
katika zahanati hiyo haikuwa shwari lakini kwa jitihada zake na
kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo
mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa
kupewa hadhi ya nyota nne.
Akiyataja mambo waliyoweza
kuyafanya katika Zahanati hiyo ni pamoja na Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa
(Ambulance), Mashine ya Kufulia,Jenereta, Choo kwa kinamama
wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashne tatu za
kupmia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.
Zahanati nyingine zilizoweza
kupandishwa hadhi Halmashauri ya Ilala ni pamoja na Zahanati ya Tabata,
Mhongo la Ndege, Kinyerezi na Kadlugambwa.
Taarifa kutoka Kamati ya Zahanati
imeeleza kuwa mwanzo zahanati yetu ilikua na nyota mbili ambapo hizo
zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota
mbili.
Kamati hiyo imewashukuru wananchi
kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimezifanyiwa kazi
na ku pelekea zahanati hiyo kupata nyota mbili za ziada, kamati
memshukuru pia Diwani Omary Said Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri,
na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.
Tags
AFYA