
Hayo yamewekwa wazi na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa na kusema Tambwe ndiyo mchezaji pekee atakaendelea kuukosa mchezo huo wa leo.
"Kwa ujumla kikosi chetu kipo vizuri kabisa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC", amesema Nsajigwa.
Amisi Tambwe amekuwa yupo nje (benchi) tokea ulipoanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na maumivu ya goti ambayo yalimuanza msimu uliopita.
Tags
yanga