BANDA MEDIA BLOG

JAMII KUFICHA TAARIFA KUMESABABISHA KASI UKATILI KWA WATOTO WILAYANI MPWAPWA

Na Stephen noel Mpwapwa
MTANDAO wa polisi wanawake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umesema kasi
ya ukatili kwa watoto inasababishwa na jamii kuficha taarifa za
vitendo hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa dawati lá njisia katika kituo cha
polisi wilayani hapa Bi Elfrida Mapunda katika maadhimisho ya miaka
kumi ya kuanzishwa kwa dawati hilo.
Bi Mapunda amesema kuwa vitendo vya ukatili vinavyodhidi kushika kasi
vinasababishwa na jamii kuzidi kuvifumbia macho vitendo hivyo au
kamalizana kienyeji bila kufuata sheria na bila kuangalia madhara.
Aidha Bi Mapunda ameitaka jamii kwa kusaidiana na jeshi lá polisi
kuweza kushirikiana katika kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na
wanawake.
Pia amesema katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao
huo kumeongezeka kwa taarifa za ukatili ambazo hapo awali zilikuwa
zinafichwa kutolewa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi Selina Chimwaga
amesema kuwa kuwa kundi kubwa lá watoto hao wenye mtindio wa ubongo
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa matibabu kutokana na kuto
kuwa na bima za afya.
Bi Chimwaga amesema watoto wengi wamekuwa wakifungiwa ndani, wengine
kunyeshwa pombe na dawa za usingiz ili kuogopa kuwaambia kwa baadhi ya
wazazi.
Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2009 kimeweza
kuwabaini zaidi ya watoto Zaid ya 5000 wenye matatizo ya utindio wa
ubongo wakiwa wanafungiwa ndani na kukosa haki yao ya Elimu na hivyo
wengi wao wakiwa watu wazima huwa tegemezi.
Mmoja wa walimu anaye fundisha elimu maalun katika shule ya Msingi
Chazugwa bwana Hussein Hussein amesema kuwa watoto wenye ulemavu wa wa
akili hufichwa ndani kutokana na Imani potofu uliopo kwa jamii juu ya
watoto hao.
Bwana Hussein alisema katika shule yake kuna wanafunzi 21 wakiwamo
wasichana 8na wavulana 13 japo kuwa wilaya ina watoto wa Namna hiyo
wengi katika wilaya ya Mpwapwa.
Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG