Raundi ya Sita ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL), itaendelea kesho Ijumaa Oktoba 20, 2017 kwa mechi za makundi yote matatu.
Katika Kundi ‘A’, Mvuvumwa FC
ya Kigoma, watacheza na Mgambo JKT katika Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam. Mvuvumwa anatumia Kanuni ya 6 (1) na (2) kuhamishia mechi zake
za nyumbani Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kutoka Uwanja wa Tanganyika,
Kigoma.
Mechi nyingine kwenye kundi hilo itafanyika Jumapili Oktoba 22, mwaka huu kwa michezo mitatu.
Mechi hizo ni kati ya Kiluvya
United na Mshikamano kwenye Uwanja wa Filbert Bayi, ilihali African
Lyon itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Friends
Rangers itapambana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.
Katika Kundi ‘B’ siku hiyo ya
Ijumaa Oktoba 20, mwaka huu Polisi Dar itacheza na Coastal Union ya
Tanga kwenye Uwanja wa Azam wakati michezo mingine katika kundi hilo
ikichezwa Jumamosi na Jumapili.
Jumamosi Mbeya Kwanza itacheza
na JKT Mlale Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani na
Jumapili Polisi Tanzania watawakaribisha KMC kwenye Uwanja wake wa
nyumbani wa Ushirika Moshi, huku Mawenzi Market ya Morogoro wakiwaalika
Mufindi United kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katika Kundi ‘C’ kutakuwa na
mchezo mmoja siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2017 Pamba SC ya Mwanza itacheza
na Alliance Schools nayo ya Mwanza kwenye Uwanja wa Nyamagana huko
Mwanza na michezo mingine itafanyika Jumamosi na Jumapili.
Michezo ya Jumamosi
itazikutanisha Biashara Mara dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa
Karume Mara,Transit Camp itakuwa mwenyeji wa Dodoma FC kwenye Uwanja wa
Kambarage Mjini Shinyanga,wakati mchezo mwingine wa Kundi C, Toto
Africans ya Mwanza itacheza na Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo
utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA WIKIENDI HII