
Kituo cha mabasi ya
mwendo kasi cha Fire kikiwa kimesimama kutoa huduma kwa abiria baada
kujaa maji kwa bonde la Jangwani na kufunika barabara kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2017.

Mbunge wa Jimbo la Ilala Iddi Azan
Zungu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika eneo la
Jangwani lilolokumbwa na mafuriko na kusababisha barabara ya Morogoro
kufungwa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha leo Oktoba 26, 2017 Jijini
Dar es salaam.
Eneo la bonde la
Jangwani likiwa limefurika na kuziba barabara ya Morogoro kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.


Barabara ya Morogoro ikiwa imefungwa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.

Gari za mwendokasi zikiwa zimesitisha
huduma kwa sasa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha leo Oktoba 26,
2017 Jijini Dar es salaam.
Tags
mvua kubwa


