
Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya
Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Nyerere Dar es Salaam, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania inakosa
watalii wengi kutokana na kukosa ndege.
"Tumenunua ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege
zingine ikiwepo Bombardier zitawasilia mwakani 2018 mwanzoni tunafanya
haya kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake
idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu
ni ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii
wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu" alisema Rais
Magufuli
Serikali ilikiri ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 Dash 8
iliyonunuliwa na serikali ambayo ilipaswa kuingia nchini toka mwezi
Julai lakini ikashindikana kufika kutokana na kudaiwa na kampuni ya
Stirling Civil Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier
Q400-Dash 8 iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada.
Tags
Bombardier