Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen (track suti ya kijani) akipimwa macho zoezi
lililoendeshwa kwa wananchi wote waliohudhuria katika maadhimisho ya
kifo baba wa Taifa, Kiwanja cha Mandela, Mjini Sumbawanga, baadaya
kupima alionekana hana tatizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen (track suti ya kijani) akiwa na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Rukwa Bernanrd Makali wakiongoza mazoezi ya viungo kwa wananchi
waliojitokeza katika kiwanja cha Nelson Mandela kuadhimisha kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa
Bernanrd Makali (track nyeusi) akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, pamoja na afisa Michezo wa Manispaa ya
Sumbawanga Adam Evarist wakiongoza mazoezi ya viungo kwa wananchi
waliojitokeza katika kiwanja cha Nelson Mandela kuadhimisha kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere.
Wananchi pamoja na watumishi
mbalimbali wa serikali walioshiriki katika kuadhimisha siku ya
kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika Kiwanja cha Nelson Mandela, Mjini
Sumbawanga.
………………….
Wananchi wa Mkoa wa Rukwa
wameshauriwa kuweka utamaduni wa kugfanya mazoezi kila siku kwa lengo la
kuyaenzi Maisha ya Hayati Baba wa Taifa, kwani kufanya hivyo ni kwa
faida ya afya zetu wenyewe.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika kuadhimisha kumbukumbu ya
kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika kiwanja wa Nelson
Mandela, mjini Sumbawanga.
Maadhimisho hayo yaliyokwenda
sambamba na jumamosi ya pili ya mazoezi pamoja na kilele cha wiki ya
vijana wananchi walijitokeza kwa wingi asubuhi kwaajili ya kushiriki
kwenye mbio zilizoanza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kuelekea kwenye
jkiwanja hicho cha mpira kikubwa mkoani Rukwa.
Amesema kuwa watanzania wameacha
kufanya mazoezi hali inayopelekea kunyemelewa na magonjwa mbalimbali
hali inayopelekea kupunguza nguvu kazi ya taifa.
Ameongeza kuwa Katika kuiweka afya
yake vizuri, hutumia dakika 20 asubuhi kufanya mazoezi kabla ya
kuelekea ofisini hali iliyopelekea kuoneka na afya nzuri mbali na kuwa
na umri mkubwa.
“Msinione bado nipo fiti ni
kwasababu ya kufanya mazoezi kila siku kwa dakika 20 kabla sijaingia
ofisini, mazoezi haya ni faida yetu wenyewewe, sio faida ya Rais, Makamu
wa Rais wala Waziri Mkuu, na Katika kuona kuwa watanzania wameacha
mazoezi Serikali ya ikaagiza kila jumamosi ya pili ya mwezi iwe ya
mazoezi si kwasababu nyingine bali ni kuendelea kutunza afya zetu,”
Alifafanua.
Pia alitumia nafasi hiyo kumuagiza
Katibu Tawala wa Mkoawa Rukwa kuhakikisha kuwa anaweka utaratibu wa
kuhakikisha kila mtumishi wa serikali anashiriki kwenye mazoezi hayo ili
kuimarisha afya zao na kuendeleza kulijenga taifa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa
Mkoa wa Rukwa Bernard Makali katika kuisemea kilelel cha wiki ya vijana,
amewataka vijana wote mkoani humo kuandika maoni juu ya fani
watakazotaka zifundishwe katika chuo kipya cha ufundi VETA
kinachotarajiwa kuanza kujengwa katika makao makuu ya Mkoa huoMjini
Sumbawanga.
“Katika kuhakikisha huduma
mbalimbali za kiufundi zinapatika katika Mkoa wetu, hivi karibuni
serikali itaanza kujenga chuoi cha ufundi VETA cha kisasa kabisa, hivyo
make tayari kwa hilo na wamekuja kutaka kutaka maoni juu ya fani ambazo
tunataka zifundishwe kwenye chuo hivyo ni fursa yenbu kuleta maoni ya
fani mnazotaka zifundiswe kwenye chuo hicho,” Alimalizia.
Tags
RC RUKWA