
Kichuya amefunga bao akiichezea Simba kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Yanga, Jumamosi hii. Kichuya alifunga bao hilo likiwa ni la kuongoza dakika ya 58 kipindi cha pili lakini halikudumu baada ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.
Ikumbukwe kuwa Oktoba 1, 2016 Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya kwanza akiwa Simba bao lake likiwa ni la kusawazisha wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.
Aidha, Februari 25, 2017 Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya pili mfululizo kwenye mechi za ligi Simba ilipopata ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.
Jumamosi ya Oktoba 28, 2017, Kichuya ameweka rekodi ya kuifunga Yanga kwa mara ya tatu mfululizo kwenye mechi za VPL mechi iliyochezwa uwanja wa Uhuru, Dar.
Tags
Kichuya