Na Samuel Samuel
Mtanange wa watani wa jadi kati ya
Yanga SC na Simba SC almaarufu kama Kariakoo derby umemaliza uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam kwa timu zote kutoshana nguvu kwa sare ya
1-1.
Alikuwa mnyama Simba SC aliyekuwa
wa kwanza kuwanyanyua maelefu ya mashabiki wake vitini kupitia kwa
Shiza. Kichuya baada ya kuicheza vyema krosi ya Emanuel Okwi. Hii
ilikuwa dakika ya 57 baada ya timu zote kwenda mapumziko zikiwa suluhu
bin suluhu.
Dakika tatu baadae Yanga waliweza
kusawazisha goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wao wa kati Obrey Chirwa
na mwisho wa mchezo matokeo kusomeka 1-1.
*TATHIMINI*
Tukianza na wenyeji wa mchezo
Yanga SC; waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-4-2 . Ukuta wa nyuma
ukiwa na walinzi wanne Juma Abdul kulia na Gadiel Mbaga kushoto
wakicheza kama walinzi wa pembeni. Kati walisimama Andrew Vicent na
nahodha Kelvin Yondani.
Eneo la kati ; Pappy Tshishimbi
kama kiungo mkabaji ambaye alikuwa akicheza kama box to box midfielder.
Alifanya kazi tatu kwa wakati mmoja , alisimama kama kiungo mkabaji timu
ikipoteza mpira , alijenga mashambulizi kati kama kiungo mchezeshaji
pia akisogea juu kama kiungo mshambuliaji. Tshishimbi alisimama kati na
Rafael Daudi . Kushoto kwao akitaradadi vizuri Geofrey Mwashiuya na
kulia Piusi Buswita ambaye leo hakucheza kama winga alisimama kama
kiungo mchezeshaji wa pembeni timu ikishambulia pia aliingia kati
kukaba.
Mbele walisimama Obrey Chirwa kama
mshambuliaji kiongozi kati na Ibrahim Ajibu akicheza kama deep
playmaker kujenga daraja la viungo wa kati na safu ya ushambuliaji na
wakati huo huo akifanya switching na Chirwa kama mshambuliaji.
Yanga walijipanga vyema kwenye
kujilinda wakifanya mashambulizi machache ya kushitukiza lakini
yaliyokuwa yamepangwa vyema hususani kipindi cha kwanza . Kama sio
umakini wa golikipa wa Simba Aishi Manula kwa mikwaju ya Tshishimbi
huenda Yanga wangepata magoli zaidi ya hilo moja .
Tshishimbi aliwatawala Simba eneo
la kati atakavyo lakini alikosa sapoti nzuri kwa Rafael Daudi ambaye
hakuwa na kasi nzuri kusharabu ubora wa Tshishimbi pale kati . Kushindwa
kwa Rafael Daudi kutengeneza kombinesheni nzuri na Tshishimbi kulifanya
mara nyingi Ajibu kushuka chini hali iliyoifanya safu ya ushambuliaji
ya Yanga kucheza mbali na lango la Simba , kusogea mbele ilihitaji
counter na sio kufungua vyumba kwa pasi fupi fupi. Lwandamina kipindi
cha pili aliliona hili kwa kumtoa Rafael Daudi na kumwingiza Pato
Ngonyani lakini Omog tayari alikuwa amemzidi kete kwa kumuingiza Jonasi
Mkude kuondoa utawala wa Tshishimbi eneo la kati baada ya kumzidi
vilivyo James Kotei.
Madhaifu ya Yanga yalikuwa kwenye ‘
pre marking ‘ . Hawakuwa wazuri sana kwenye kumkaba mtu asiye na mpira .
Zaidi ya mara tano Shiza Kichuya alipokea mpira akiwa huru . Goli lake
baada ya krosi ya Emanuel Okwi, hakuwekewa tena ulinzi wa kutosha kabla
yakuwa na mpira hali iliyompa uhuru wa kufunga akiwa mbele ya lango la
Yanga .
Pia kukosa umakini wa kutumia
nafasi za kufunga , dakika ya 82 Emanuel Martin alishindwa kuipatia
Yanga SC goli la wazi akiwa yeye na kipa .
Kwa ujumla Yanga wamefunguka
lakini kuna nafasi wanakosa watu wenye uwezo mzuri kwa asilimia 100
mathalani kiungo wa kutengeneza kombinesheni na Tshishimbi hususani
kwenye offensive patterns. Kama Yanga wangekuwa na Kamusoko ni dhahiri
timu isingecheza sana chini kwa maana ya kufunguka zaidi wakitoka box
moja kwenda jingine . Pressing kwenye wings haikuwa kubwa kama
ilivyozoeleka kwa Saimoni Msuva lakini kizuri Lwandamina amejua kumtumia
Buswita kama mchezeshaji kwenye wings pia akivunjikia ndani kusaidia
kukaba.
SIMBA SC
Moja ya kitu ambacho Simba
watajilaumu leo ni kushindwa kufatilia maendeleo ya Yanga katika mechi
zao saba za awali kabla ya leo. Walishindwa pia kuheshimu uwezo wa
George Lwandamina katika kusoma wapinzani wake .
Simba waliingia uwanjani na hali
ya kujiamini sana kitu ambacho kiliwanyima ‘ command ya mchezo ‘ (
authority ). Walianza na mfumo wa 4-4-2 kama Yanga lakini battling ya
Tshishimbi na Kotei pale kati iliwafanya kugeuka na kucheza 4-2-3-1 ili
kujaribu kupunguza pressure ya Pappy Kabamba Tshishimbi hali iliyomfanya
Haruna kurudi chini kidogo kusaidia kuendesha timu huku Mavugo akibaki
kama mshambuliaji pekee mbele ndio maana Simba kipindi cha kwanza
walikuwa na possession kubwa lakini hawakuweza kufika langoni kwa Yanga
kwa shambulio la maana hata moja .
Kuchagua kumwanzisha James Kotei
mbele ya Tshishimbi haukuwa uchaguzi mzuri kutokana na Kotei kutokuwa
mzuri sana kwenye battling za kusogeza timu juu katika upinzani mkali .
Omog alitakiwa kumwanzisha Jonasi Mkude toka mwanzo akiwa na Mzamiru
Yassin au Saidi Ndemla ambaye mara nyingi amekuwa akiamua matokeo katika
mechi za watani wa jadi.
Hakutaka kubadilika kwenye mipango
yake ya kutumia wing ya kulia kupitia Erasto Nyoni na Shiza Kichuya
kushambulia. Ni zaidi ya mechi tatu anatumia mfumo huo kitu ambacho
Yanga waliking’amua kwa kutanua kiungo kuziba njia sema walikuwa na
makosa kumlinda Shiza Kichuya ambaye alikuwa anafanya switching mara kwa
mara ya kuhama kutoka box moja kwenda jingine.
Kizuri kwa Simba SC ni uwezo wa
kumiliki mpira , kuwa vyema katika kujenga mashambulizi lakini mipango
yao haikuwa mizuri kwenye finishing kutokana na tempo ya mechi .
Goli lao dakika ya 57 ni goli
nzuri ambalo lilisukwa vyema toka wing ya kushoto kwa Okwi na kutumia
vyema makosa ya walinzi wa Yanga katika kumlinda Kichuya lakini
wakashindwa kulinda goli kwa kuruhusu mashambulizi ndani ya 18 yao .
Mipango mingi ilikuwa ni kumzibia njia Ibrahim Ajibu lakini wakamsahau
Chirwa .
Endapo Simba itashindwa kucheza
kwa kasi , kuheshimu uzito wa jezi yao , kuwa na uwezo wa kumsoma
mpinzani wake wanaweza kujikuta wanapotea kwenye harakati za ubingwa
hususani duru la pili la ligi.
Ukiitazama ni timu ambayo ina
makosa machache ya kiufundi hususani nidhamu ya mchezo na jinsi ya
kutumia wachezaji waliopo pia kujengeka vyema katika saikolojia ya
kusaka ushindi .
Tags
‘KARIAKOO DERBY’