
Mapema leo ametua uwanja wa ndege wa jeshi wa ManyameAkaunti ya chama
cha Zanu PF inasemama kuwa Emmerson Mnangagwa amefanywa kuwa rais wa
mpito.
Mnangawa mwenye umri wa miaka 75 alifutwa kama makamuu wa rais kutokana na kile serikali ilisema kuwa kutokuwa mtiifu.
Kufutwa kwake kulionekana kama nia ya kumwezesha mke wa Rais Mugabe,
Grace, kufuata nyayo za mumewe na kuwa kiongozi wa Zimbabwe.
Awali alikuwa ametoa wito kwa mumewe kumfuta makamu wa rais.
Bw. Mnangagwa ambaye ni mku wa zamani wa ujasusi amekuwa mtu ambaye alitarajiwa kumrithi Rais Mugabe 93.
Kufutwa kwake kulimaanisha kuwa Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa kuwa
makamu wa rais wakati wa mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF
mwezi ujao..
Wakati huo huo jeshi linamshikilia waziri wa fedha Ignatius Chombo,
Waziri wa Elimu Prof. Jonahan Moyo Afisa Mwandamizi ndani ya chama cha
ZANU-PF Savior Kasukuwere
Tags
Zimbabwe ya Mugabe