Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limetoa onyo kali kwa magazeti
na Wahariri wa gazeti la Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa la
kuchapisha na kusambaza mwenendo wa shauri lililokuwa likifanyiwa kazi
na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.