Libya yaanzisha uchunguzi kuhusu biashara ya utumwa
Naibu
Mkuu wa Baraza la Uongozi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya
amesema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu suala la kushikiliwa na kuuzwa
wahajiri kama watumwa karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.Ahmed Maiteeq amesema kuwa, serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imeiagiza kamati iliyoundwa kuchunguza uuzaji wa wahajiri wa Kiafrika kama watumwa nchini humo ili kuwatia mbaroni na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa magendo ya binadamu.
Wakazi wa Paris mji mkuu wa Ufaransa karibu elfu moja juzi usiku waliandamana kulalamikia magendo hayo ya binadamu na kuuzwa wahajiri kama watumwa huko Libya.
Tags
UTUMWA