MSHAMBULIAJI mpya wa Klabu Bingwa
ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Bernard Arthur, tayari amewasili
nchini leo Jumapili alfajiri akitokea Ghana.
Mara baada tu ya kutua kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), Arthur
ameweka wazi kuwa amekuja kuisaidia timu hiyo kumaliza kwenye nafasi
nzuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiwemo kutwaa
ubingwa.
“Malengo yangu ni kujiunga na
kuendeleza niliyofanya nchini Ghana kwa kuyaleta hapa natarajia mambo
mazuri kama kila kitu kitakwenda vizuri kama unavyojua mambo ya mpira
wakati mwingine kuna kupanda na kushuka yote haya ni fomu si unajua
namna ya kuipata fomu.
“Nitajitahidi kujiweka vizuri,
nitjitahidi kufanya mazuri kwa klabu, na kufanya mazuri binafsi, kufunga
mabao kadhaa kama sitofunga basi angalau kutoa pasi nzuri za mabao na
kuisaidia klabu kuwa kwenye nafasi nzuri na kutwaa taji la ligi,”
alisema Arthur.
Arthur alisema anasmhukuru
Mwenyezi Mungu kwa kufanikiwa kujiunga na klabu bora ya Azam FC huku
akidai hiyo ni njia sahihi ya kufikia malengo yake.
“Kwanza napenda kumshukuru
Mwenyezi Mungu kufika salama Tanzania na najisikia vizuri kujiunga na
klabu hii ya ajabu yenye baadhi ya historia nzuri…Nimeijua Azam FC
kupitia wachezaji wenu Yakubu (Mohammed), Razak (Abalora) ambao ni
rafiki zangu mmojawapo nilicheza naye Razak wameniambia kuhusu klabu.
“Ofa ilipokuja sikujiuliza
chochote kuhusu kujiunga nayo, nafikiri kujiunga na Azam FC ni jambo
zuri kwangu na zuri kwa kipaji changu na maendeleo yangu na timu pia,”
alisema.
Mshambuliaji huyo anayesifika kwa
kushambulia kwa spidi, kupiga mashuti, kufunga mabao na kusumbua mabeki,
amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 11 kwenye msimu ulioisha wa Ligi Kuu
Ghana (GPL), ambapo mbali na kuichezea Liberty pia amewahi kupita WAFA
SC ambayo iliwahi kumpeleka kwa mkopo kwa vigogo wa Ivory Coast, Asec
Mimosa.
Sapraizi nyingine inakuja
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul
Mohamed, aliyeambatana na mchezaji huyo akitokea Ghana alipokwenda
kufanya usajili wake aliweka wazi kuwa huenda kabla ya kumalizika kwa
wiki ijayo timu hiyo ikafanya maajabu mengine katika usajili wa dirisha
dogo unaoendelea hivi sasa utakaomalizika Desemba 15 mwaka huu.
“Kwanza niseme tu kwamba binafsi
naweza nikasema ni moja kati ya usajili ambao naimani nao, unajua wakati
mwingine kwenye usajili mashabiki lazima waelewe hiki kitu kwenye
usajili ni gambling (bahati nasibu), yaani unaweza ukasajili mtu anawika
sana lakini akija anakuwa hafanikiwi ama unaweza ukasajili mtu wa
kawaida sana halafu akija anafanikiwa.
“Sasa usajili wa Bernard Arthur ni
moja kati ya usajili ambao mimi binafsi nauona kwamba unanipa matumaini
kwa kile ambacho tulikuwa tunakitafuta, tunatafuta mtu ambaye ni
mfungaji lakini ni zaidi ya mchezeshaji,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Pengine labda
kabla ya wiki haijaisha hii inayoanza Jumatatu basi tutafanya maajabu
mengine na tuombe Mungu na huenda sapraizi ikaja, sapraizi itakuja kuna
watu walikuwa wanaona tulikuwa Ghana, Zambia Kitwe, tumerudi sasa
tunarudi tena Zambia na huenda hili la Zambia safari hii wale wote ambao
walikuwa wanasema tukawaambia tumemaliza twendeni tukacheze mpira
Tags
usajili wa wachezaji