Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi wa masuala ya Ukimwi kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI wakati wa
warsha ya wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba 14,
2017.
Mkurugenzi wa Utafiti na Tathimini
Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela
akiwasilisha mada ya hali ya UKIMWI nchini kwa Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi wakati wa warsha kwa
wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika tarehe 14 Novemba, 2017.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya
Taifa ya kudhibiti Ukimwi Dr. Leonard Maboko akichangia hoja kuhusu
masuala ya Ukimwi wakati wa Warsha ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Masuala ya UKIMWI iliyofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Daniel Mtuka akifafanua jambo wakati wa
warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu masuala ya Ukimwi nchini
iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba 14, 2017.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Martha Mlata akichangia hoja
wakati wa warsha iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi
kuhusu masuala ya Ukimwi iliyofanyika Mjini Dodoma.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe.Zainab Bullu akifafanua jambo
wakati wa warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo iliyoandaliwa na Tume ya
Taifa ya kudhibiti Ukimwi.
Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu – Dodoma
…………..
Na.MWANDISHI WETU
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume
ya Taifa yakudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imedhamiria kuendelea kuwajengea
Uwezo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi ili
iweze kushiriki vyema katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Akizungumza wakati wa Semina ya
siku tatu iliyoanza leo mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vita dhidi ya janga
la Ukimwi inafanikiwa ili kulinda nguvu kazi ya Taifa.
“Serikali imejipanga kuhakikisha
swala hili linapewa kipaumbele hasa katika kutoa elimu kwa wananchi ili
waweze kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI”
Alisisistiza Mhe. Mhagama
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema
kuwa vita dhidi ya janga la Ukimwi niya kila Mtanzania hivyo ni vyema
wadau wote wakashirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi Mhe. Daniel Mtuka
amesema Warsha hiyo inajenga msingi kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika
kutekeleza majukumu yake.
Aliongeza kuwa Wajumbe wa Kamati
hiyo wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na Ukimwi hapa
nchini ili kuhakikisha kuwa malengo yakuondoa janga hilo hapa nchini
yanatimizwa kwa wakati muafaka.
Kwa Upande wake mmoja wa wajumbe
wa Kamati hiyo Mhe. Martha Mlata amesema kuwa ni wakati muafaka sasa kwa
jamii kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya Janga la Ukimwi kwa
kusimamia maadili katika Jamii hali itakayochochea kuleta mabadiliko.
Warsha ya Siku tatu kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi inafanyika mjini Dodoma
kwa siku tatu ikilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili
waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.