NA RAMADHANI JUMA
OFISI YA MKURUGENZI
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Dodoma imeajiri askari Mgambo 30 watakaokuwa wanafanya doria katika viunga
vya Mji ili kudhibiti watu wanaochafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ikiwa ni
namna mojawapo ya kuhakikisha mji huo unakuwa safi wakati wote ikizingatiwa
ndiyo Makao Makuu ya Nchi.
Hatua hiyo inafuatia
kampeni ya usafi wa mazingira iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Daktari Binilith
Mahenge ya kufanya usafi siku ya Jumamosi kila wiki.
Akizungumza wakati wa zoezi
la usafi mwishoni mwa Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin
Kunambi amesema askari Mgambo 30 waliofuzu mafunzo wako tayari na kwamba
Manispaa inatarajia kuanza kuwatumia wiki hii ya kwanza ya mwezi Desemba.
Aliwashauri wakazi wa
Dodoma na wageni kujiepusha na utupaji wa taka ovyo, na kwamba atakayebainika
na kuthibitika kufanya hivyo atatozwa faini kati ya Shilingi 50,000 hadi
300,000 kulingana na mazingira ya tukio papo hapo na endapo atashindwa kulipa
atatumikia kifungo cha miezi sita gerezani.
Tags
USAFI WA MAZINGIRA