Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akihutubia wakati akizindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020 wa Bohari ya Dawa (MSD) jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa SMD, Sako Mwakalobo, akielezea mpango huo mbele ya mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya.
uzinduzi ukiendelea.
Viongozi wa idara mbalimbali wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Mpoki Ulisubisya, akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD)imezindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini.
Akizindua
mpango mkakati huo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
ameipongeza MSD kwa kuandaa upya mpango huo ambao wamejikosoa na
kuboresha maeneo muhimu ili kuendana na vipaumbele vya serikali na
mahitaji ya wananchi wa Tanzania, hususan vituo vya Afya vya Umma.
Maeneo
hayo muhimu ni pamoja na Kujitegemea kifedha, kuuhuisha Mnyororo wa
Ugavi, Kuboresha mfumo wa Tehama, Matumizi yenye tija ya Rasilimali
Watu, Utawala na
Ushirikishwaji wadau.
Katika
hatua nyingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya ameingia mkataba maalumu wa
utendaji kazi (Performance Contract)na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean
Bwanakunu ili kuhakikisha utekelezwaji wa haraka wa Mpango mkakati
uliozinduliwa.
Aidha
katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema
atahakikisha Mpango Mkakati 2017-2020 unatekelezwa ambapo kila
Mkurugenzi na Mameneja wa MSD wameingia mikataba inayopimika ya
utendaji kazi.
Bwanakunu
aliongeza kuwa ufuatiliaji wa utendaji utafanywa kupitia Ofisi maalumu
ya kusimamia utekelezaji wa mikakati ya MSD(Strategic Management
Office)Tayari kila Mkurugenzi na mameneja wa MSD wamesaini mkataba
kutekeleza Mpango Mkakati huo wa Kati.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
Tags
MCD