BANDA MEDIA BLOG

JUMLA YA WANAWAKE 556 HUPOTEZA MAISHA KWA VIFO VINAVYOTOKANA NA UZAZI.



Mkurungezi idara ya Uuguzi na Ukunga Nchini Dr Gustan Moyo akifungua mkutano wa Wauguzi na Wakunga wa  kanda za Ziwa na Magharibi Uchechemevu wa Ajira.

 Imeelezwa kuwa jumla ya wanawake 556 kwa mwaka 2015/16 kwa kila vizazi hai laki moja hupoteza Maisha kutokana na vifo vitokanavyo na uzazi ambapo takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2010 vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 454.

Hayo yamesemwa na mkurungezi idara ya uuguzi na ukunga nchini Dr Gustan Moyo kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya afya, wakati akifungua mkutano Wa uchehchemuzi (ADVOCACY) ya ajira kwa wauguzi na wakunga kwa kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi ulifanyika Leo mjini hapa.
Mkurungezi idara ya Uuguzi na Ukunga Nchini Dr Gustan Moyo mwenye koti jeusi pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya uuguzi na ukunga Wizara ya Afya Dkt, Ndementria Vermand wakiwa katika mkutano huo [PICHA ZOTE NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]

Dr Moyo amesema takwimu za kuhusu watumishi Wa afya kwa mwaka (2012/2013) zinaonyesha kuwa ni asilimia 55 ya wafanyakazi Wa afya ndio wanaotoa huduma vijijini na maeneo yasiyofikiwa kiurahisi ambao kuna zaidi ya asilimia 75 ya watanzania.
Hata hivyo amesema ili kukabiliana na tatizo la upungufu Wa wauguzi na wakunga wizara ya ya afya kwa kushirikiana na mradiwa more and better midwives for rural Tanzania wamejipanga Kuelimisha jamii na wanafunzi Wa sekondari juu ya kuitambua fani ya uuguzi pamoja na mchango wake katika huduma ya afya ya uzazi ya mama na mtoto, na kushawishi vijana wanaohitimu Elimu ya sekondari kusomea gani ya uuguzi na ukunga.
Wauguzi na Wakunga wakiwa kwenye mkutano huo

Pia kuviwezesha vyuo vya uuguzi na ukunga ili kutoa wauguzi wakunga wenye weledi na ujuzi stahiki katika utoaji Wa huduma mbalimbali za afya hasa za mama na mtoto.
Aidha ameongeza kuwa serikali imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo hivi karibu ilitoa ajira 3000 katika kuongeza idadi ya watumishi lakini pamoja na hayo amesema upungufu Wa Wa wafanyakazi Wa afya hususani wauguzi na wakunga.
Naye mwakilishi wa Amref Dr Aisa Nkya Muya Amesema ili kutatua tatizo hilo shirikiano ni muhimu kwa wadau na serikali kuungana na kupeana mawazo jinsi yakufanya ili kukabiliana na suala hilo.
Mkuu wa Miradi wa Amref  Nchini Aisa Muya akifafanua Jambo wakati alipokuwa akiongea na Wauguzi na Wakunga wa kanda ya  Ziwa na ya Magharibi kwa ajili ya Uchechemevu [ADVOCACY] ya ajira.

Mradi huo ni Wa miaka mitano tokea mwaka (2016_2021 lengo ku  la mradi huo nikuboresha afya na ustawi Wa akina mama na watoto.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG