Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde
amewahakikishia wafanyabiashara wadogo wadogo wa stendi ya mabasi ya
vijijini katika eneo la Kikuyu Kusini juu ya ujenzi wa soko kwa ajili ya
matunda na mboga mboga na kuondokana na adha ya kufanya biashara katika
maeneo ambayo siyo rasmi.

Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu kero za wafanyabiashara hao alipotembelea stendi ya mabasi hiyo eneo la Kikuyu Kusini na kuwahakikishia wafanyabiashara hao juu ya ujenzi na ukamilishaji wa soko ambalo litagharimu kiasi cha Shilioni Milioni Tisini na Mbili(92,000,000)

Aidha katika Mkutano wa hadhara wa wananchi Kikuyu Kusini,Mh Mavunde amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wao katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kikuyu B ambapo Mbunge huyo ameahidi kuwachangia matofali 500 na mifuko ya saruji 50.

Wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini wamempongeza Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya za kuwaletea maendeleo na kumuahidi kumpa ushirikiano katika uongozi wake.

Tags
MAVUNDE