Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli jana tarehe 07 Desemba, 2017 aliwasili Mkoani Dodoma ambako
pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za
maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru zitakazofanyika katika uwanja wa
Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi tarehe 09 Desemba, 2017.

Katika Ikulu ya Chamwino, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge.
Akiwa Mkoani Dodoma Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni rasmi katika shughuli mbalimbali za kiserikali.
Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.

Tags
9 DESEMBA 2017