Hii hapa ni video ya hali kile alichokisema wakati akizungumza na wanafunzi wa NASULI SEKONDARI
………………………………………………………
NA DITHA NYONI
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekanusha taarifa zilizozagaa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa amepinga marafuku wananchi wa mkoa wa
Ruvuma wasiitane baby.
Tamko hilo amelitoa wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ndogo ya mkoa wa Ruvuma ,
hii inakuja baadaya ya taarifa kuzagaa na yenye picha inayoonesha
mavazi tofauti na eneo alilokuwa anatoa ujumbe katika shule ya sekondari
NASULI na MBAMBA BAY huku ujumbe ukisomeka “marukuku kuitana baby” mkuu
wa mkoa wa Ruvuma.
Ikumbukwe Novemba 8 mwaka huu,
mkuu wa mkoa wa Ruvuma alifanya ziara katika halimashauri ya natumbo
katika shule ya sekondari nasuli na kuzungumza na wanafunzi hao, huku
kampeni kubwa ili kuwa ni kueneza ujumbe wa kumtaka mwanafunzi wa kike
kuvaa maguni manne ambayo ni sare ya shule,joho la maafari,gauni la
harusi,na matreniti dress
“ili muweze kufanikisha masomo
yenu watoto wakike lazima mvae magauni ili muweze kufanikisha malengo
yenu”pia mkuu wa mkoa wa Ruvuma aliongeza kuwa ni marafuku watoto wa
kiume na wakike kuitana baby
“msikubali kuitwa baby kwa sababu
kukubali kuitwa baby ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi,mskubali
kuitwa queen we ni mwanafunzi unatafuta maisha na wala usikubali kuitwa
mrembo au mzuri alisema Rc MNDEME.
Lengo ya kampeni ni kumsaidia mwanafunzi wa kike aweze kufikia ndoto zake za kielimu na kuweza kufanikisha malengo yake.
Kufatia taarifa hizo mkuu wa mkoa
alisema ilikuwa inawalenga wanafunzi wa kike na sio watu wazima kwani
taarifa zinazoenezwa na makundi ya watu wachache zinalengo la kupotosha
umma hivyo wakazi wa mkoa wa Ruvuma wapaswa kupuuzia
Aidha amewataka wazazi na jamii
kwa ujumla kutumia kauli mbiu hiyo ya magauni manne ili iwe chachu kwa
wanafunzi wa kike waweze kufanikisha ndoto zake,kwani wanaofanya hivyo
hawana nia nzuri wa watoto wa kike
Tags
MNDEME