BANDA MEDIA BLOG

REAL MADRID USO KWA USO NA PSG,BARCELONA NA CHELSEA 16 BORA LIGI YA MABINGWA


4736BD1200000578-5167063-image-a-29_1512994232611
 
TIMU za Barcelona na zitaendeleza upinzani wao wa muda mrefu kwenye michuano ya Ulaya baada ya kupangwa pamoja katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kikosi cha Antonio Conte kilizidiwa kete kileleni mwa Kundi C na Roma na sasa kitasafiri kwenda Nou Camp kwa mchezo wa mtoano. 
Tottenham iliyovuna pointi nyingi zaidi kihistoria msimu huu, itamenyana na mabingwa wa Italia, Juventus, waliomaliza nyuma ya Barcelona kwenye Kundi D.
Vibara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamepangiwa timu nafuu kidogo Basle, wakati Liverpool baada ya kuongoza Kundi E itamenyana na Porto.
Hii inakuwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2003-2004 timu tano kutoka nchi moja kuingia hatua ya mtoano. 
Timu nyingine ya England katika hatua hii, Manchester United itamenyana na Sevilla ya Hispania kuwania tiketi ya Robo Fainali. 
Katika droo iliyopangwa leo, mabingwa watetezi, Real Madrid watamenyana na Paris Saint-Germain.
Chelsea na Barcelona zimekutana mara 15 kwenye michuano ya Ulaya, kila timu ikishinda mechi tano na nyingine tano zimetoka sare. 
Mechi za kwanza za 16b Bora zitachezwa Februari 13 na 14 na Februari 20 na 21, wakati marudiano yatakuwa Machi 6 na 7 na Machi 13 na 14.

RATIBA 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA 

Juventus vs Tottenham
Basle vs Manchester City 
Porto vs Liverpool
Sevilla vs Manchester United
Real Madrid vs Paris Saint-Germain
Shakhtar Donetsk vs Roma 
Chelsea vs Barcelona 
Bayern Munich vs Besiktas  
(Mechi za kwanza zitachezwa Februari 13/14 na Februari 20/21. Marudiano yatakuwa Machi 6/7 ma Machi 13/14)

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG