BANDA MEDIA BLOG

“Save” haya majina na 2018 waangalie watakavyoishangaza dunia


2017 ndio huoo umebakiza siku chache kuisha huku Kylian Mbappe akiwa jina lililoushtua ulimwengu, lakini 2018 kuna vijana wadogo ambao wanaweza kufanya kile Mbappe alichofanya 2017.

1.Phil Foden,ana miaka 17 raia wa Uingereza na tayari msimu huu katika mechi kadhaa alionekana akiwa benchi la Man City, Pep ameanza kuona ukubwa wa Foden na katika fainali za vijana under 17 alifunga mara mbili.

2.Justin Kluivert, pengine kwa sasa anazungumziwa sana huku akihusishwa na kwenda Manchester United, mtoto wa nyota wa zamani wa Barca Patrick Kluivert anatajwa kama nyota tishio zaidi katika siku za usoni
.
3.Ferran Torres, ni habari kubwa nchini Hispania na huyu ndio mchezaji wa kwanza kuzaliwa kuanzia mwaka 2000 na kucheza La Liga, mkataba wake na Valencia unakaribia kuisha huku Barcelona na Real Madrid wakifuatilia kwa karibu hatma yake.
4.Jadon Sancho, alizaliwa mwaka 2000 akakulia kituo cha kulea wachezaji cha Man City na baadae aliamua kutafuta timu, alizitosa United na Chelsea baadae akatua Dortmund ambako anapewa nafasi kumrithi Dembele na tayari watabiri wa mambo wanasema Sancho ni almasi kubwa ijayo katika soka.
5.Ethan Ampadu, inajulikana kwamba Antonio Conte haamini watoto huwa anapenda wazee wa kazi, lakini sio kwa Ampadu ambaye ana miaka 17 tu huku tayari Conte ameshampa nafasi na anaonekana kumkubali, ni kijana ambaye anaweza kuwa lulu mpya Chelsea.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG