Wema ambaye alitangaza kuihama CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kupata misukosuko ya tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya, ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Wema amewahi kushinda taji la Miss Tanzania ameweka picha akiwa amevaa nguzo za chama hicho tawala nchini Tanzania na kuandika haya:
“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani…. #ThereIsNoPlaceLikeHome… Feels good to be Back…”
Tags
Wema Sepetu
