Kamati ya Utendaji ya
Yanga leo imetangaza kuunda kamati mpya ya mashindano,ambapo nafasi ya
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Hussein Nyika huku makamu wake akiteuliwa
Samuel Kumay.
Mmoja wa wajumbe walio kati hiyo ni Shija Richard ambaye aligombea Urais wa TFF lakini akashindwa na Wallace Karia.
Wajumbe wengine
katika kamati hiyo yenye watu 23 ni Omary Chuma,Hussein Ndama, Majid
Seleiman, Mussa Katabaro,Yusuphed Mhandeni, Beda Tindwa na Jackson
Maagi.
Wengine
watakaoisaidia kamati hiyo ni Lameck Nyambaya, Nicko Meela, Edward Urio,
Rogers Gumbo, Ediger Mutani, Sanga Kayanda Hamad Islam, Pascal Kihanga
na Isiaka Sengo.
Pia kuna wangine kama Bahati Mwaseba,Rashid Msinde Khalfani Kigwelembe,Yanga Makanga Rogers Lamlembe na Leonald Chiganga.
Tags
yanga
