BANDA MEDIA BLOG

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI ZA MITAA [TALGWU] KIMESHANGAZWA NA SERIKALI KUTOA KIPAUMBELE CHA KULIPA MADENI YA WALIMU HUKU WAO WAKIACHWA ILIHALI MADENI YAO NI ZAIDI YA 37.5 BIL.








Wajumbe wa kikao cha Baraza kuu la wafanyakazi wa Serikali za Mitaaa TALGWU kilichofanyika mjini Dodoma [PICHA NA JOHN BANDA]




Chama cha wafanyakazi wa serikali  za mitaa TALGWU kimesikitishwa na serikali kulipa deni la  walimu na kuwasahau wao wanaoidai serikali jumla ya shilingi bilioni 37.5 .
Ofisa Habari wa  TALGWU Shani Kigwasali,amesema kuwa deni hilo ni la siku nyingi na limekuwa likiongezeka kila mwaka kutokana na mahitaji muhimu ya wafanyakazi ikiwemo suala la ugonjwa  na likizo.

Amesema wanashangazwa kuona walimu wanalipwa na wao  wafanyakazi wa serikali za mitaa bao sio walimu kusahaulika kwani wao ndio wanaoshugulikia mambo yote ya maendeleo katika halmashauri ikiwamo ukusanyaji was mapato na ujenzi wa shule.

naibu waziri wa kazi ajira na vijana mh Antony Mavundeambaye alikuwa mgeni rasmi  amesema serikali itahakikisha inalipa madeni ya watumishi hao lakini  amewataka watumishi hao kutojihusisha na udanganyifu wowote kwani serikali haitamfumbia macho Mtu yeyote atakayejihusisha na udanganyifu huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG