Waziri wa Mawasiliano wa Utawala Haramu wa Israel, Ayoob Kara ametishia kuwanyonga waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo hivyo ndani ya utawala huo.
Kara ametoa vitisho hivyo katika kongamano la kila mwaka la chama chake mjini Eilat, kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kusisitiza kwamba, kunaandaliwa sheria muhimu kuhusiana na vyombo vya habari. Ameongeza kwa kusema kuwa, kutekelezwa kwa sheria hizo mpya kutasaidia kudhibiti zaidi vyombo vya habari na chombo kitakachokiuka sheria hizo kitakabiliwa na adhabu kali ikiwemo kunyongwa muhusika wake.
Tags
israel