Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya Michael Mtaite amesema sababu ya kumnyima dhamana mshtakiwa Mh. Mbilinyi na mwenzake ambaye ni katibu wa CHADEMA kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga ni hofu ya mshtakiwa kutohudhuira mahakamani mara kwa mara na pia anataka kesi hiyo isikilizwe siku chache na kwa mfufulizo iwe imekwisha.
"Mahakama inataka kusikiliza kesi hii kwa muda mfupi sana, ndani ya wiki moja kuanzia jumatatu iwe imeshakwisha, hivyo tunawataka washtakiwa kurudi rumande" alisema Mtaite
Sugu na mwezake wanashtakiwa kwa kutoa lugha za uchocheza na za fedhiha kwa Rais Magufuli mnamo tarehe 30,Desemba mwaka jana katika viwanja vya mwenge jijini mbeya.